Habari
MHE. SIMBACHAWENE AMTEMBELEA MAMA SITTI MWINYI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amemtembelea Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, 2024.
“Rais, amenielekeza kuwafikishia salaam zake na amesema yuko pamoja nanyi na ndio mana amenituma kufika hapa nyumbani na kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi” amesema Mhe. Simbachawene.
Mhe. Simbachawene amesema Rais Mhe. Dkt. Samia anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Aidha, Mama Sitti amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote bila kuchoka na amemuombea kwa Mungu aendelee kutumia hekima na busara katika kuiongoza Tanzania.