Habari
MHE. SIMBACHAWENE AIPONGEZA WHI KWA KUENDELEA KUJENGA MAKAZI BORA YA WATUMISHI , ASISITIZA KUJENGA ZAIDI KARIBU NA MAENEO YA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa nyumba zilizojengwa na WHI eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Bw. Xavier Daudi.