Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MHE. RIDHIWANI KIKWETE AOMBA USHIRIKIANO KUTIMIZA LENGO LA MHE. RAIS LA KUWA NA SERA ZA KIUTUMISHI NA MIUNDO YENYE TIJA KWA USTAWI WA TAIFA


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo  kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi.