Habari
MHE. RIDHIWANI KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA IDARA YA TEHAMA SERIKALINI IKIWA NI MWENDELEZO WA VIKAO KAZI VYAKE VYA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA OFISI YAKE

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.