Habari
MHE. NDEJEMBI AKEMEA TABIA YA WIZI KWA WATUMISHI INAYOKINZANA NA DHAMIRA YA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN YA KUJENGA UADILIFU

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Ilala (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma walio katika wilaya hiyo.