Habari
MHE.KIKWETE : TAALUMA YA UUGUZI NI YA KUJITOA NA YENYE UTHUBUTU

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wauguzi wa Mkoa wa Pwani kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani ambapo amewahimiza Wauguzi hao kuwahudumia wananchi na jamii yote ya Kitanzania kwa moyo na upendo wa hali ya juu.