Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MHE. KIKWETE AKAGUA SHAMBA LA PARACHICHI IRINGA


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amepokea na kuikaribisha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria  kukagua mradi wa shamba la matunda ya Parachichi.

Mradi huo unaotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji Cha Ibumila Wilaya ya Iringa, Mkoa Iringa.

Mhe. Kikwete ameeleza Kamati hiyo kuwa kupitia TASAF Kijiji hicho kimeweza kuibua mradi wa uanzishaji wa shamba la matunda ya Parachichi ekari tatu yenye jumla ya miche ya 231. Mradi huo umekamilika na kukabidhiwa kwa uongozi  ambapo wanafunzi wa Kijiji hicho wanapata elimu kwa vitendo.

Ameongeza kuwa Shamba hili limekuwa shamba darasa kwa jamii pia ambapo wanajamii wanaozunguka shamba hili wamepata fursa na sehemu ya kujifunza.

Aidha, Mhe. Kikwete amemshukuru Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa ruzuku kwa walengwa kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini. Mpango huu umekuwa mkombozi wa kaya nyingi zenye Hali duni.