Habari
TPSC NA TAASISI YA UONGOZI ZATAKIWA KUANDAA PROGRAMU ZA MAFUNZO ZITAKAZOBORESHA UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI WA UMMA NA VIONGOZI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo.