Habari
MHE. KIKWETE AELEKEZA VIBALI VYA MAOMBI YA WATUMISHI WANAOSTAHILI KUPANDA MADARAJA YAWASILISHWE OFISI YA RAIS – UTUMISHI ILI YAFANYIWE KAZI KWA HARAKA

Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.