Habari
MHE. JENISTA AWATAKA VIONGOZI NA WATENDAJI SERIKALINI KUSIMAMIA KIKAMILIFU RASILIMALIWATU ILI KUEPUSHA MIGOGORO SEHEMU ZA KAZI KWA USTAWI WA TAIFA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikaribishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa, alipowasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.