Habari
MHE. JENISTA ATEMBELEA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YAKE KUJIRIDHISHA NA UTOAJI WA HUDUMA KULINGANA NA FEDHA INAYOTOLEWA NA SERIKALI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing, Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista iliyolenga kujiridhisha na utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kama unaendana na fedha iliyotolewa na Serikali kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.