Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MAONI NA USHAURI WA WAKURUGENZI KUBORESHA RASILIMALIWATU SERIKALINI


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Veila Shoo ametoa rai kwa Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali kutoa maoni na ushauri kwa uhuru na uwazi ili kuboresha matokeo ya zoezi la tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Bi. Veila ametoa rai hiyo wakati akiwasilisha mada katika Kikao kazi cha kujadili matokeo ya zoezi la tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kinachofanyika kwa siku mbili tarehe 17 na 18 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa wakati wa maandalizi ya Kikao kazi hicho, Sekretarieti ilifanya jitihada za kuhakikisha inachagua viongozi wenye uzoefu wa aina tofauti ili kuboresha zaidi Taarifa hiyo kwa lengo la kukamilika na kutumiwa na Taasisi katika uandaaji wa IKAMA ya mwaka 2025/26.

Aidha, alibainisha shughuli za kikao kazi hicho ikiwa ni pamoja na kuwa na mawasilisho ya jumla na mahsusi ambayo yatakuwa na majadiliano kwa kila wasilisho ili kutoa nafasi ya kujadili, kutoa maoni na ushauri wa namna ya kuboresha usimamizi na ukuaji wa Utumishi wa Umma.

Pia, alitumia fursa ya kikao kazi hicho kuwashukuru Wakuu wa Taasisi wote waliotoa ushirikiano stahiki wakati zoezi ambapo matokeo yake yameonekana na Serikali inayafanyia kazi.