Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI KWA WATUMISHI WA UMMA KUONGEZA UFANISI


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Leila Mavika amesema mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watumishi wa umma ni muhimu kwa kuwa yanaongeza uelewa wa kutambua, kuchambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaj kazi wa shughuli za Serikali.

Bi. Mavika ameyasema hayo Aprili 27, 2026 wakati akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi katika kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wa Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.

Bi. Mavika meongeza kuwa, kutokana na uelewa ambao umepatikana wakati wa mafunzo hayo ni imani yake kuwa kila mtumishi wa ofisi hiyo atakuwa na uwezo wa kuchambua na kutambua vihatarishi vilivyopo katika eneo lake la kazi na kuvidhibiti kabla ya madhara kutokea.

Awali, Afisa Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando amesema, Serikali imeweka msisitizo kwa Wizara na Taasisi za umma kuimarisha mifumo ya udhibiti wa vihatarishi ili kuboresha uwajibikaji.

Vilevile Bi. Lugando alitoa wito kwa watumishi wa kila Idara na vitengo kuhakikishe wanatambua vihatarishi vinavyoweza kutokea katika Idara na vitengo vyao ili kuimarisha usalama.