Habari
MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026
Wananchi na Watumishi kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania mnakaribishwa kuja kupata huduma katika mabanda ya maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma leo tarehe 18 Juni 2026.
Kupitia maadhimisho hayo, mtapata fursa ya kuhudumiwa papo kwa papo, kupata elimu kuhusu huduma za Serikali, kuwasilisha maoni yenu na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu huduma za umma.
Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea viwanja vya maonesho ili kujionea huduma zinazotolewa na kunufaika na fursa ya kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi kutoka kwa wataalamu wa wizara na Taasisi mbalimbali za umma.
