Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA NA VITENGO VYA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU KATIKA WIZARA NA IDARA ZINAZOJITEGEMEA, WAKALA WA SERIKALI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA, SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA


Kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kinahitimishwa leo tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray.

kikao hicho  kilifunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo katika siku hizo tatu washiriki wamepewa uelewa wa namna ya kuimarisha utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.