Habari
KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA NA VITENGO VYA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU KATIKA WIZARA NA IDARA ZINAZOJITEGEMEA, WAKALA WA SERIKALI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA, SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi akizungumza katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa, leo Juni 2, 2026 jijini Dodoma.
Kikao kazi hicho cha siku tatu, kimefunguliwa Juni mosi, 2026 na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo Mhe. Ridhiwani Kikwete na kinatarajiwa kufungwa kesho na Naibu Waziri Ofisi ya Rais UTUMISHI Mhe. Regina Qwaray (Mb).
Aidha, kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Sikivu, Jumuishi, Wenye Matokeo na Uwajibikaji kuelekea Dira 2050”.
