Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KATIBU MKUU, UTUMISHI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA JICA


 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora. 

 

Kikao hicho kimefanyika  leo Ijumaa Novemba 8, 2024  katika Ofisi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

 

Miongoni mwa masuala waliyojadili ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi pamoja na maombi  ya vibali vya ajira  kwa raia wa kutoka Japan wanaokuja kufanya kazi nchini katika miradi ya Serikali katika Utumishi wa Umma  ambapo fursa  hiyo huwasaidia Wazawa kubaki na ujuzi  unaoweza kutumika hata baada ya miradi ya maendeleo kukamilika 

 

Aidha, viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe.  Shigeru Ishiba.