Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE, APONGEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Mkomi, amepongeza utoaji wa huduma zinazotolewa kwa Watumishi wa Umma na Wananchi ambapo amewahimiza kufika katika maonesho hayo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

“Nashukuru nami nimepata nafasi ya kufika katika viwanja hivi kuona shughuli na huduma mbalimbali ambazo zinatolewa katika viwanja hivi, nipongeze waandaaji wa Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane), huduma zinazotolewa ni nyingi hivyo niwahimize Watumishi wa Umma na Wananchi kufika katika maonesho hayo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali”, amesema Bw. Mkomi