Habari
KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, ATOA SHUKRANI KWA USHIRIKI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametembelea mabanda ya Wizara na Taasisi za Umma ili kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hizo pamoja na kutoa shukrani kwa ushiriki mkubwa katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025.
“Ninapongeza na kutoa shukrani nyingi kwa Wizara na Taasisi zote za Umma zilizoshiriki katika Maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma, zimeonesha ushirikiano mkubwa na idadi ya ushiriki imekuwa kubwa,” amesema Bw. Mkomi
Bw. Mkomi ameseongeza kuwa, kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya Wizara na Taasisi pamoja na kupata mrejesho wa utendaji kazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma.
Aidha, Katibu Mkuu Mkomi ameendelea kutoa wito kwa Watumishi wa Umma, Wananchi na Wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ili kupata huduma mbalimbali.