Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KATIBU MKUU MKOMI AFURAHISHWA NA TAASISI KUJITOKEZA KWA WINGI KUTOA HUDUMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amefurahishwa na Taasisi za Umma kujitokeza kwa wingi kushiriki na kutoa huduma za Kiserikali papo kwa hapo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea Maonesho hayo.

Bw. Mkomi ameyasema hayo wakati alipotembelea mabanda na kujionea huduma zikitolewa na Wizara na Taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye maonesho hayo yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Maonesho hayo yaliyoanza Juni 16 yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya kesho Juni 23, ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.

Maadhimisho na Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa yameratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo Kaulimbiu ya Mwaka huu ni “Kuwezesha kwa Utumishi wa Umma uliojikita kwa Umma wa Afrika ya Karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi; Ni Safari ya Mafunzo na Mabadiliko ya Kiteknolojia”.