Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KARIBU TUKUHUDUMIE: WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 inatoa huduma za kiutumishi katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2025.

Hivyo, Watumishi wa Umma na Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la ofisi hiyo ili kupata huduma mbalimbali za kiutumishi.

Baadhi ya huduma hizo ni Mifumo ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, e-Watumishi (HCMIS), e-Msawazo (HR-Assessment), e-Uhamisho (Watumishi Portal), e-      Mikopo, e-Utendaji, e-Likizo na e-Mrejesho.

 Kadhalika, ofisi kwa kushirikiana na viongozi wengine watashughulikia masuala ya PEPMIS.

Aidha katika banda hilo zitatolewa huduma nyingine mathalani huduma za kisheria katika Utumishi wa Umma.