Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA YARIDHISHWA NA JITIHADA ZA MLENGWA WA TASAF WILAYANI UYUI NA KUMCHANGIA 530,000/= KUMUWEZESHA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA KUISHI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria kwa upendo waliouonyesha kwa mlengwa wa TASAF, katika Kata ya Migiri Wilayani Uyui Bi. Amina Abdallah kwa mchango wa kumuwezesha mlengwa huyo kukamilisha ujenzi wa nyumba aliyoanza kuijenga kutokana na ruzuku ya TASAF anayoipata.