Habari
KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA SEKRETARIETI YA AJIRA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha michakato ya ajira inafanyika kwa ufanisi na kwa uwazi wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Septemba 2024 hadi Januari 2025.
Mhe. Dkt. Mhagama mesema kitendo cha usaili kufanyika katika ngazi za mikoa badala ya kuwalazimu waombaji kazi wote kufika jijini Dodoma kumeleta ahueni kubwa kwa waombaji kazi hao hususani wale waliotoka kwenye familia maskini.
Hapo awali wazazi walilazimika kuuza ardhi au ngombe ili kijana wao aweze kusafiri kuja jijini Dodoma kwa ajili ya kufanya usaili ila ubunifu wa kufanya usaili kimkoa umerahisishia. Amesema Mhe. Dkt. Mhagama amesema
Amesisitiza kuwa utaratibu huo umeondoa usumbufu pamoja na kumfanya Muombaji kazi kutokutumia gharama ya usafiri kwa ajili ya kufika jijini Dodoma kufanya usaili
Akizungumzia matumizi ya mfumo wa Ajira Portal kwa waombaji kazi Mhe.Dkt. Mhagama amesema mfumo juo umeondoa dhana ya upendeleo wa kupata ajira katika Utumishi wa Umma na kuchagiza ushindani miongoni mwa waombaji kwani hutoi fursa ya kuonana ana kwa ana na wahusika
Nimekuwa nikipokea simu nyingi kutoka kwa Watoto wa familia masikini wa kutoka vijijini wakiwa wamepata ajira serikalini pasipo kumjua yeyote aliyepo serikalini amesisitiza Mhe.Dkt. Mhagama
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amesema ajira katika Utumishi wa Umma zinapatikana kwa ushindani kutokana na idadi kubwa ya wasomi iliyopo lakini nafasi ni chache
Ametumia fursa hiyo kuwaomba Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Mabalozi wa Sekretariet ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa kuwaeleza wananchi kuwa ajira katika Utumishi wa Umma hazihitaji kumjua yeyote na cha msingi ni kufuata taratibu zilizowekwa na Sekretarieti hiyo wakati wa kuomba kazi.