Habari
KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA IMEJIPANGA KIKAMILIFU KUISIMAMIA OFISI YA RAIS-UTUMISHI

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga kuiwezesha kamati hiyo kupokea wasilisho la muundo na majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.