Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGENEZA MIPANGO MKAKATI


“Andaeni Mpango Mkakati wa Halmashauri kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 na Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs)”

Hayo yamesemwa na Afisa kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Oswin Mkinga wakati akitoa mafunzo maalum (Mobile clinic) ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara, Vitengo na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Iringa kuhusu mfumo wa e-Utendaji (PEPMIS) katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Machi 12, 2026.

Aliongeza kuwa, iwapo masuala yaliyoainishwa katika nyaraka hizo yataingizwa katika mpango mkakati wa Halmashauri, halmashauri itatekeleza majukumu yake na kutoa huduma kwa umma kwa ufanisi.

Pia, alisema kuwa watumishi wa halmashauri hiyo watakuwa na uwezo wa kujaza kwenye mfumo wa e-Utendaji kwa takwimu ambazo zinauhalisi na zenye kueleweka.