Habari
FURSA ZA MAFUNZO KWA WATANZANIA NJE YA NCHI NI MATOKEO YA MAHUSIANO MAZURI YA KIDIPLOMASIA YANAYOJENGWA NA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na watumishi wa umma walionufaika na mafunzo nchini Korea yanayofadhiliwa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Serikali ya Korea (KOICA) mara baada ya watumishi hao kumtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.