Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyanyua mkono) akizungumza jambo wakati Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikikagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Kijiji cha Makunda, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida. Wengine ni Watumishi wa Zahanati ya Makunda.