Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WATUMISHI WALIOZALIWA MWEZI NOVEMBA WASHUKURU


Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Cosmas Ngangaji amemshukuru Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw. Musa Magufuli kwa ubunifu wake na kuweka utaratibu wa kuwapongeza na kuwatakia kila la kheri watumishi wake kwa kuzingatia mwezi waliozaliwa.

“Kwa niaba ya watumishi wenzangu tuliozaliwa mwezi Novemba ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wetu Bw. Juma Mkomi, tunashukuru kwa motisha hii ya kufanya tukio la kumbukizi ya kuzaliwa kwetu kwa pamoja na kufurahi na watumishi wenzetu” alisema Bw. Ngangaji

Aliongeza kuwa tabia njema huonekana kama ni ya kawaida, lakini kwa tukio hili haina budi kupongeza wote waliofanikisha jitihada hizi zenye kufurahisha jamii.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya  Anuai za Jamii kutoka Ofisi ya Rais- UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo amewasisitiza wazaliwa wote wa mwezi Novemba kuzingatia mafunzo waliyopata leo kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na uwekezaji kwa kuwa ni kipimo cha utu ambacho kinatakiwa kufikiwa na kila mmoja.

Aidha, amewapongeza wote waliozaliwa mwezi Novemba na kuwatakia kila la kheri katika kumbukizi ya kuzaliwa kwao na kuwaomba waendelee kutumikia familia zao na taifa kwa ufanisi.