Habari
WATUMISHI OFISI YA RAIS-UTUMISHI WACHANGIA DAMU KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KULINDA RASILIMALIWATU NCHINI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwahamasisha watumishi wa ofisi yake kuchangia damu katika Kituo Kidogo cha Damu Salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini ACP. Ibrahim Mahumi na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mikataba ya Utendaji kazi Serikalini Bi. Zainabu Kutengezah.