Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

WANAWAKE WA OFISI YA RAIS - UTUMISHI WAUNGANA WANAWAKE WENGINE WA DODOMA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE  DUNIANI 


 

Watumishi wanawake kutoka   Ofisi ya Rais - UTUMISHI wameungana na wanawake wengine  wa Jiji la  Dodoma   katika kusheherekea  Siku ya   Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka. 

Maadhimisho hayo ambayo Kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali  katika  wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma yakiwa yamebeba Kauli mbiu isemayo   "Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo  ya Taifa  na ustawi  wa jamii"

Siku hii ni muhimu kwa wanawake kwani  huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii.

Wanawake wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI  wanaadhimisha siku hii muhimu huku wakikumbushana juu ya umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wananchi .