Habari
WANANCHI TUMIENI HATIMILIKI ZA KIMILA MNAZOZIPATA KUPITIA MKURABITA KUJIKWAMUA KIUCHUMI-Mhe. Jenista

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisoma maandishi ya uzinduzi wa jengo la masijala ya ardhi lililojengwa na MKURABITA katika Kijiji cha Maweni, Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha mara baada ya kuzindua rasmi masijala hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za MKURABITA katika Halmashauri hiyo. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella pamoja na watendaji wengine wa Serikali.