Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

UTUMISHI YATWAA UBINGWA WA MPIRA WA MIGUU SHIMIWI KWA MARA NYINGINE.


Timu ya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Utumishi FC) imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Wakala wa Serikali (SHIMIWI) kwa upande wa mpira wa miguu, baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mikwaju ya penati ambapo Utumishi ilibuka kidedea kwa Penati 4-2 dhidi ya wapinzani wake Tume ua Umwagiliaji katika mchezo wa fainali uliochezwa Septemba 15, 2025 jijini Mwanza.

Ikumbuke Ocktoba 5, 2024 Utumishi FC ilitwaa ubingwa wake kwa mara ya kwanza Mkoani Morogoro ambapo mashindano ya SHIMWI 2024 yalifanyika.

Hii ni mara nyingine tena kwa Utumishi FC kuandika historia ya kuwa miongoni mwa timu zenye mafanikio makubwa zaidi katika mashindano haya, hatua inayodhihirisha ubora, mshikamano na nidhamu ya hali ya juu waliyonayo wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Ushindi huo unaiweka Utumishi kwenye rekodi ya kuwa miongoni mwa timu chache zilizoonesha ubora wa kudumu, kwani ni mara nyingine tena wanatwaa kombe hilo, wakionesha nidhamu ya mchezo, mshikamano na umahiri mkubwa uwanjani.