Habari
UTUMISHI YATIMBA FAINALI SHIMIWI 2025

Timu ya Ofisi ya Rais – Utumishi imeendelea kung’ara katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2025 baada ya kutinga fainali kwa kishindo.
Utumishi ilipata ushindi wa bao Moja dhidi ya Takukuru Septemba 13, 2025 katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo nusu fainali ya mpira wa miguu ilirindima.
Safari ya Utumishi kuelekea hatua ya juu kabisa ya mashindano haya imeonyesha uimara, mshikamano na nidhamu ya hali ya juu ya michezo, ambapo wamefanikiwa kuwashinda wapinzani wao kwenye hatua za awali hadi nusu fainali.
Mashabiki wa timu hiyo wameeleza kufurahishwa na mafanikio hayo, wakisisitiza kuwa ushindi huu ni ishara ya mshikamani na juhudi kubwa zinazowekwa na wachezaji pamoja na viongozi wao.
Kwa hatua hii, macho yote yameelekezwa kwenye fainali ya SHIMIWI 2025, ambapo Utumishi itamenyana na mpinzani wake kwa lengo la kutwaa ubingwa na kuandika historia nyingine ya michezo ndani ya Utumishi wa Umma.