Habari
UTUMISHI SC YAIPASUA 3–0 RAS ARUSHA SHIMIWI 2026
Timu ya Utumishi Sports Club (Utumishi SC) imeendelea na mwendo wake katika Mashindano ya SHIMIWI 2026 yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3–0 dhidi ya RAS Arusha.
Leo Septemba 28, 2026 katika Kiwanja Magereza Utumishi SC imepata ushindi mnono na kuendelea kuonesha kiwango kizuri cha Utumishi SC katika mashindano ya SHIMIWI yanayoshirikisha timu mbalimbali za Serikali.
Utumishi SC ilianza maandalizi ya SHIMIWI 2026 kwa msisitizo wa nidhamu, mshikamano, heshima na uadilifu, kama alivyosisitiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. Juma Mkomi, wakati wa kuwaaga wanamichezo hao.
