Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

TIMU YA WANAWAKE YA RIADHA OFISI YA RAIS - UTUMISHI YAINGIA FAINALI KATIKA MBIO ZA KUPOKEZANA


 

Timu ya wanawake ya riadha ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI imefanikiwa kutinga hatua ya fainali katika mbio za kupokezana (relay) kwenye mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2025 yanayoendelea jijini Mwanza.

Wanariadha wa Utumishi walionesha kasi ya hali ya juu katika mbio za nusu fainali, hatua iliyowapa tiketi ya moja kwa moja ya kucheza fainali, wakibeba matumaini ya kutwaa ubingwa wa mwaka huu.

Kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Bw. Hassan Shaibu, mafanikio hayo yametokana na nidhamu ya hali ya juu ya wachezaji, mazoezi ya mara kwa mara na umoja ndani ya kikosi, huku akibainisha kuwa morali ya ushindi imeendelea kuwa kubwa zaidi kadri mashindano yanavyosonga mbele.

Wanawake wa Utumishi sasa wanasubiri kumenyana na timu pinzani katika fainali ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na kiwango walichokionyesha katika hatua zilizopita.