Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

TIMU YA RIADHA YA WANAWAKE UTUMISHI YATWAA UBINGWA WA MBIO ZA KUPOKEZANA


Timu ya riadha ya wanawake ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI imeibuka kidedea leo tarehe 11 Septemba, 2025 baada ya kutwaa ubingwa wa mbio za kupokezana (relay) katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 

Wanariadha wa Utumishi walionesha uwezo mkubwa na mshikamano wa kiufundi uliopelekea kushinda kwa kishindo na kuwapiku wapinzani wao waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo.

 

Ushindi huu unaongeza heshima kwa Utumishi, ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika michezo mbalimbali, ikiwa ni kielelezo cha juhudi za kujenga mshikamo na afya bora kwa watumishi wa umma kupitia michezo.