Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

TIMU YA MPIRA WA PETE UTUMISHI SC YAICHAPA RAS MARA 63–0


Timu ya Mpira wa Pete ya Utumishi Sports Club (Utumishi SC) imeendelea kuonesha kiwango bora katika mashindano ya SHIMIWI 2026 yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 63–0 dhidi ya RAS Mara.

Mchezo huo umefanyika leo, Septemba 27, 2026, katika Viwanja vya Moshi Club, Mkoani Kilimanjaro, ukiwa ni mchezo wa tatu kwa timu ya Utumishi SC katika mashindano hayo.

Utumishi SC ilitawala mchezo huo tangu mwanzo hadi mwisho, ikionesha kiwango kizuri, ushirikiano na umakini katika kila idara ya mchezo, hali iliyoiwezesha kupata ushindi huo wa magoli 63 bila kuruhusu RAS Mara kupata bao.

Ushindi huo unaendeleza mwendo wa Utumishi SC katika Mashindano ya SHIMIWI 2026, huku timu hiyo ikiendelea kupambana kutimiza malengo yake na kufanya vizuri katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu mbalimbali kutoka taasisi za Serikali.

Utumishi SC — Umoja Kazini, Ushindi Uwanjani!