Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

TIMU YA MPIRA WA MIGUU OFISI YA RAIS - UTUMISHI YATINGA ROBO FAINALI.


Timu ya mpira wa miguu ya Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini Mwanza.

UTUMISHI walipata nafasi hiyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani na kujikusanyia alama muhimu katika michezo ya hatua za makundi dhidi ya Timu ya Mahakama, hali iliyowafanya kufuzu na kuendelea na safari ya kuwania ubingwa wa mwaka huu 2025.

Mashindano ya SHIMIWI 2025 yamehusisha timu mbalimbali kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujenga mshikamano na kudumisha afya za watumishi kupitia michezo ikiwa na kauli mbiu "Michezo kwa Watumishi, Huongeza Tija Kazini, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu".

Akizungumza mara baada ya mchezo uliowapa tiketi ya kuingia robo fainali, nahodha wa timu hiyo, Bw. Gimonge Chacha alisema “ushindi huo ni matokeo ya mshikamano, nidhamu ya hali ya juu na maandalizi ya muda mrefu”.

Timu ya Ofisi ya Rais - UTUMISHI sasa inajiandaa kukutana na wapinzani wao katika hatua ya robo fainali, huku wachezaji na mashabiki wakionyesha matumaini makubwa na timu yao kuwa itaendelea kufanya vizuri zaidi na hata kutwaa ubingwa wa SHIMIWI 2025.