Habari
TAKUKURU YATAKIWA KUTOA MAFUNZO YA PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI KWA WATENDAJI WA KATA ILI WASHIRIKI KIKAMILIFU MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kufungua mafunzo ya Programu ya TAKUKURU RAFIKI kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) yaliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) jijini Dodoma.