Habari
SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI YATAKIWA KUYAFANYIA KAZI KWA UADILIFU NA WELEDI MALALAMIKO YA WANANCHI DHIDI YA VIONGOZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwaongoza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuimba wimbo wa mshikamano daima ikiwa ni sehemu ya kuhimiza uwajibikaji kwa wajumbe wa baraza hilo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.