Habari
OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWAPA MATUMAINI WENYE UHITAJI KWA KUTOA MSAADA WA KIJAMII

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi akielekea kuwasalimia wazee na watoto wanaotunzwa katika Nyumba ya Amani na Furaha Hombolo kwa lengo la kutoa msaada wa kijamii katika kituo hicho. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro pamoja na watendaji wengine wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.