Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. SENYAMULE ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA RAIS-UTUMISHI


 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule leo Alhamisi  Machi 07,  2024 ametembelea Banda la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo katika  Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma ambako Maonesho ya Wiki ya Wanawake yanafanyika kwa muda siku tano kuanzia leo.

Mhe. Senyamule pamoja na mambo mengine ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kushiriki katika Maonesho hayo huku akiitaka itoe huduma nzuri  kwa  Watanzania ili kukidhi ndoto ya Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia Watanzania wote kwa usawa.

Tanzania inaungana na nchi nyingi Duniani katika kuadhimisha  Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila mwaka  Machi 8, 2024 kwa kuthamini na kutambua mchango wa wanawake katika ujenzi wa jamii na taifa bora kiujumla