Habari
MHE. WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA KUSIMAMIA SUALA LA NIDHAMU KWA WATUMISHI WAO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, Bi. Hapiness Msanga akiwasilisha taarifa ya hali ya Watumishi katika Wilaya yake kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.