Habari
MHE. SIMBACHAWENE AKUTANA NA WENZA WA VIONGOZI WA KITAIFA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo tarehe 30 Julai, 2024 kwa nyakati tofauti amewatembelea na kufanya mazungumzo Mama Anna Mkapa na Mama Janeth Magufuli katika makazi yao Osterbay Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yake na wenza wa viongozi hao, Mhe. Simbachawene ameahidi kuwaelekeza watendaji katika ofisi yake, kushughulikia changamoto zinazojitokeza na kuwafanya wenza wa viongozi hao kuendelee kuishi kwa amani na usalama.
Aidha, Mama Mkapa amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya kumtembelea, kumjulia hali na kusikiliza changamoto alizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Vilevile Mama Janeth Magufuli amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake na kuwatunza wakati wote bila kuchoka na amemuombea kwa Mungu aendelee kuiongoza vyema Tanzania.