Habari
MHE. NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI KUTOHOFIA KUELEZA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO ILI ZITATULIWE KAMA MHE. RAIS ALIVYOELEKEZA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi, Manispaa ya Lindi na wa taasisi za umma mkoani humo wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.