Habari
MHE. JENISTA ATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA MKOANI ARUSHA KUTUMIA KITUO JUMUISHI CHA URASIMISHAJI NA UENDELEZAJI WA BIASHARA ILI KUKUZA BIASHARA ZAO NA KUONGEZA PATO LA TAIFA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajasiriamali wanaopata huduma katika kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichopo katika Kata ya Kati, Mtaa wa Pangani Halmashauri ya Jiji la Arusha alipokuwa akizindua rasmi kituo hicho akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani Arusha.