Habari
MHE. JENISTA ASISITIZA UTEKELEZAJI MKAKATI WA KUSHUGHULIKIA RUFAA ZA WATUMISHI NA WA KUZUIA ONGEZEKO LA MASHAURI YA KINIDHAMU

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama (Aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya tume hiyo kilichofanyika jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu, Idara ya Rufaa na Malalamiko, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. John Mbisso.