Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

MAKTABA YA UONGOZI KUCHOCHEA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI KATIKA KULITUMIKIA TAIFA - Mhe. Jenista


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizindua toleo la Kiswahili la tawasifu ya Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa “Maisha Yangu, Kusudi Langu” katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Anayeshiriki nae ni Mke wa Hayati Benjamin William Mkapa, Mama Anna. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue (kushoto) ambaye ameshiriki kutafsiri kitabu hicho.