Habari
MAAFISA BAJETI WAPATIWA MAFUNZO YA UMUHIMU WA UFUATILIAJI NA TATHMINI ILI KUHAKIKISHA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2026/2027 YA OFISI YA RAIS-UTUMISHI INATEKELEZWA KWA UFANISI
Mkurugenzi wa Mipango kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Bajeti wa Ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha Maafisa hao kilicholenga kuandaa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2026/2027 kilichofanyika mkoani Manyara. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, wa ofisi hiyo Bw. Patrick Allute.
