Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Habari

KIKWETE APOKEA RIPOTI YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TRAMPA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete Septemba 1, 2026 ofisini kwake Mtumba, Dodoma amepokea ripoti ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA)

Baada ya kupokea ripoti hiyo, ametoa rai kwa viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanahamasisha wanachama wengi kushiriki Mkutano huo ambao hufanyika mara moja tu kwa mwaka.

TRAMPA inawachama takribani 9000 ambapo kati ya hao, wanachama wapatao 4000 wanatarajiwa kushiriki Mkutano huo.

TRAMPA inawakutanisha na kuwaunganisha wataalamu na watunza kumbukumbu na nyaraka nchini Tanzania wanaofanya kazi katika sekta ya Umma na sekta binafsi.

Mkutano huo utaongozwa na kaulimbiu isemayo "Kumbukumbu ni Uhai wa Taasisi na Mwanga wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050".